Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Abdullah Abdullah, ambaye anaongoza pia Baraza la Ushauri kwa ajili ya amani ya Afghanistan amebainisha kuwa, duru hiyo ya kwanza ya mazungumzo ya kurejesha amani nchini humo imepangwa ifanyike siku tatu baada ya kuachiwa huru wafungwa wote wa kundi la Taliban.
Mkuu wa Baraza Kuu la Maslahi ya Taifa la Afghanistan ameongeza kuwa, akthari ya washiriki wa kikao cha baraza la ushauri wanataka kuwepo na hakikisho la kimataifa kwamba wafungwa hatari wa kundi la Taliban ambao wataachiwa huru hawatarudi tena kwenye medani za vita dhidi ya serikali ya Afghanistan.
Akihutubia mwishoni mwa kikao cha kamati tano za Baraza la Ushauri kwa ajili ya amani ya Afghanistan, Abdullah Abdullah amesema, wafungwa wote mia nne hatari wa kundi la Taliban ni raia wa nchi hiyo, na hakuna yeyote miongoni mwao ambaye ni raia wa kigeni.
Kamati za utendaji za Baraza la Ushauri, linalojulikana pia kama Loya Jirga, ambazo zilikutana jana Jumamosi, zilipiga kura za 'ndiyo' kuidhinisha uamuzi wa serikali ya Kabul wa kuwaachia huru wafungwa 400 wa kundi la Taliban.
Ijapokuwa kikao cha Baraza la Ushauri kwa ajili ya amani ya Afghanistan kilikuwa kimepangwa kiendelee kwa muda wa siku mbili, lakini hafla ya ufungaji wa kikao hicho inatazamiwa kufanyika leo Jumapili.../
342/